SERIKALI ya Afrika Kusini imewarejesha makwao raia wa kigeni 2,745 waliokuwa nchini humo kinyume cha sheria ndani ya kipindi cha wiki moja.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini amesema hatua hiyo imekuja baada ya Rais Cyril Ramaphosa kuahidi kuimarisha mapambano dhidi ya Uhamiaji haramu na kuimarisha usimamizi wa mipaka ya nchi.
Mamlaka zinasema Operesheni hizo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuhakikisha Sheria za Uhamiaji zinaheshimiwa, huku zikilenga pia kuimarisha usalama na kudhibiti shughuli za watu wanaoishi nchini bila vibali halali.
Hatua hiyo imeibua mjadala nchini Afrika Kusini kuhusu changamoto za Uhamiaji haramu na athari zake kwa ajira, huduma za kijamii na usalama wa taifa.