KATIKA mwendelezo wa dhamira ya kukuza utafiti nchini, kampuni ya Barrick nchini imekuwa mdhamini mkuu wa maadhimisho ya kumi ya wiki ya Utafiti na Uvumbuzi uliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo pia imetoa zawadi kwa washindi watatu wa miradi ya ubunifu pia imetunukiwa cheti cha tuzo kutokana na udhamini huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Katika maadhimisho ya mwaka huu imetoa kiasi cha shilingi 22 millioni kama zawadi kwa watafiti 3 walioandika miradi iliyoshinda kwenye kada mbalimbali za afya , teknolojia na ulinzi wa teknolojia kwenye jamii.
Barrick mbali na udhamini huo imekuwa katika maadhimisho ya mwaka huu imesaini mkataba wa makubaliano na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo itatoa msaada wa dola milioni 10 katika kusaidia kufanikisha kuwajengea uwezo wanafunzi,wanataaluma na uwezeshaji tafiti mbalimbali hususani zinazohusu ukuzaji wa tasnia ya madini.
Pia Barrick imewafadhili wanafunzi watano wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam kusoma shahada ya kwanza ya elimu ya madini na Jiolojia katika Chuo Kikuu cha Jahannesburg nchini Afrika ya Kusini kupitia program yake ya kuwezesha wasomi vijana inayotekelezwa kanda ya Afrika Mashariki na kati.
Kupitia uwekezaji wake Barrick imekuwa kinara kwa kuwa na dhamira ya kujenga kizazi cha wataalamu wa kuendeleza sekta ya madini nchini ambapo imekuwa ikifadhili program mbalimbali za kuwapatia Watanzania elimu na program za kuwajengea uwezo kwa vitendo na inazo programu za mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wanaosoma katika vyuo vikuu na vya kati kwenye migodi yake nchini ya North Mara na Bulyanhulu ambayo inaiendesha kwa ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals pia imekuwa kila mwaka ikifadhili semina za kuwajengea wanafunzi wa vyuo vikuu uwezo kupitia taasisi ya AIESEC Tanzania.