MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Babati mkoani Manyara, imetoa zuio la muda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuchukua hatua zozote kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Mwandishi WEtu, Manyara … (endelea).
Amri ya zuio hilo la upande mmoja (ex parte temporary prohibitory) limetolewa Jumatatu 25 Mei 2026 na Jaji Irvin Mugeta alipotoa uamuzi mdogo katika maombi ya kupatiwa kibali cha kufungua maombi ya kupata amri ya kukataza au zuio.
Maombi hayo namba 12812 ya 2026 yamefunguliwa na Katibu Mkuu wa Chadema pamoja na Bodi ya Wadhamini ya chama hicho dhidi ya Msajili, kutokana na barua ya Msajili aliyokiandikia chama hicho 7 Mei 2026 ikikitaka chama hicho kijieleze.