WAKILI wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu , Willium Maduhu ameulalamikia mwenendo wa kesi ya ugaidi inayomkabili Nestory Nkindikwa ‘Kijana Mzalendo’, kwamba inaendesha bila kufuata taratibu na wenye kumnyima haki kamili ya uwakilishi mtuhumiwa.Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza na MwanaHALISI Digital, Wakili Maduhu amesema kuwa jana tarehe 5 Oktoba kesi hiyo iliitwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kibaha ambapo mawakili wa Nkindikwa hawakumuona mtuhumiwa akiletwa wala kujuzwa kuhusu shauri hilo.
“Kwa kuwa mimi mwenyewe ambaye muungoza jopo la mawakili wanaomwakilisha mtuhumiwa nilimtuma wakili mwenzangu asimamie shauri hilo nikamwambia basi nenda kwa Hakimu akuone umefika lakini alipofika ameshuhudia shauri hilo likiahirishwa na kwamba lilikuwa likiendeshwa kwa njia ya mtandao.
Ameongeza ” Kuendesha shauri kwa njia ya mtandao sio utashi wa mahakama binafsi lazima utokane uamuzi baada ya maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo,”.
Wakili Maduhu amesema kuwa hakuna wakili yoyote aliyepewa taarifa juu ya kuendeshwa kwa shauri kwa njia ya mtandao.
Wakati huo huo Wakili Maduhu, amesema kuwa shauri hilo limegubikwa na usiri nzito kuanzia kuhamishwa kwa mtuhumiwa kutoka magereza ya Mkuza Kibaha, mpaka Segerea jijini Dar es Salaam.