ALIYEKUWA Rais wa Benin, Patrice Talon, amechaguliwa kuwa Spika wa Seneti ya nchi hiyo, miezi mitatu tu baada ya kumaliza rasmi kipindi chake cha uongozi.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Talon alichaguliwa na kuidhinishwa katika kikao cha kwanza cha Seneti kilichofanyika jijini Porto-Novo, ambapo alipata kura 24 kati ya 25 katika uchaguzi uliofanyika kwa kura ya siri.
Ushindi wake haukuwa wa kushangaza kwa wananchi wengi wa Benin, kutokana na kupewa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi tangu kabla ya uchaguzi huo kufanyika.
Kwa upande mwingine, aliyekuwa Rais wa Benin na kiongozi wa upinzani, Boni Yayi, alitarajia kuwania nafasi hiyo lakini hakufanikiwa kupata uungwaji mkono wa kutosha.
Kwa kuchaguliwa kwake, Talon ataiongoza Seneti kwa kipindi cha miaka mitano ijayo,Chombo hicho kinatarajiwa kukutana mara nne kwa mwaka kujadili masuala muhimu yanayohusu siasa, sheria na maendeleo ya taifa.
Akizungumza baada ya ushindi huo, Spika mpya wa Seneti, Patrice Talon, aliahidi kutumia kipindi chake cha uongozi kuimarisha umoja wa kitaifa, kulinda amani na kuendeleza misingi ya demokrasia nchini Benin.