NCHI wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) zimempigia kura ya kumuondoa madarakani mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo, Karim Khan, baada ya kubainika kuwa alifanya makosa ya kinidhamu na kukiuka wajibu wake.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Uamuzi huo umetolewa jana Ijumaa 24 Julai 2026 baada ya wajumbe wengi kati ya nchi 125 wanachama wa ICC kuunga mkono mapendekezo ya kumuondoa Khan yaliyotolewa na ofisi ya utendaji ya chombo kinachosimamia mahakama hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya ICC, kura 82 za nchi wanachama ziliunga mkono uamuzi huo, huku Rais wa Baraza la Nchi Wanachama wa ICC, Paivi Kaukoranta, akitangaza kuondolewa kwa Khan.
“Baraza limeamua kwa kura nyingi za nchi 82 wanachama kwamba afisa huyo aliyechaguliwa, mwendesha mashtaka Karim Khan, amefanya makosa makubwa ya kinidhamu na kukiuka wajibu wake, hivyo kuondolewa katika nafasi hiyo,” amesema Kaukoranta.
Khan mwenye umri wa miaka 56, ambaye ni raia wa Uingereza, amekanusha tuhuma hizo, huku wakili wake, Tayab Ali, akisema mteja wake atapinga uamuzi huo kupitia njia zote za kisheria zilizopo.