WAZIRI Mkuu wa Tanzania Mwigulu Nchemba, ametangaza oparesheni mpya ya kusafisha utumishi wa umma nchini, akiamuru wizara zinazohusu utumishi wa umma kuhakikisha watumishi wote katika ofisi za umma wanavaa lebo zenye majina yao kamili kwenye sare au nguo zao ili kuwatambua, kuwawajibisha, na kuwafukuza kazi mara moja wale wote wanaofanya “nyodo” na dharau kwa wananchi.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Akizungumza na wakazi wa Isimani mkoani Iringa Mwigulu amekemea tabia ya baadhi ya watumishi kuwazungusha na kuwanyanyasa wananchi, akitaja vitendo hivyo kama “ushamba” unaorudisha nyuma maendeleo ya nchi.
Waziri Mkuu amesisitiza kuwa serikali haina uhaba wa rasilimali watu, hivyo watumishi wabadhirifu na wazembe wasihamishwe vituo vya kazi, bali wafukuzwe mara moja ili kupisha maelfu ya Watanzania waadilifu wenye nia ya kutumikia umma.