BURUNDI imepanda nafasi hadi ya 119 kati ya nchi 180 katika orodha ya mwaka 2026 ya Uhuru wa Vyombo vya habari iliyotolewa na Shirika la Waandishi wa habari wasiokuwa na mipaka (RSF) Hii ikiwa ni ongezeko la nafasi sita ikilinganishwa na mwaka 2025 ambapo nchi hiyo ilikuwa ya 125.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …(endelea).
Licha ya mafanikio hayo madogo, RSF inaonya kuwa bado kuna changamoto nyingi zinazoikabili Burundi katika sekta ya habari. Shirika hilo linaeleza kuwa wanahabari wanakumbwa na shinikizo la kisiasa, kufuatiliwa kisheria pamoja na kuwepo kwa sheria zinazoweza kuzuia uhuru wa uandishi wa habari, hasa katika nyakati nyeti.
Pamoja na hayo, wanahabari wengi bado wanalalamikia mazingira magumu ya kazi, yakijumuisha kujizuia kuripoti baadhi ya masuala pamoja na changamoto za kifedha zinazoathiri vyombo vya habari binafsi.
Ripoti mpya ya Shirika la (RSF) imeonyesha viwango vya Uhuru wa Vyombo vya habari katika nchi nane za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Kenya ikiwa ya kwanza katika kanda kwa kushika nafasi ya 106 na kupata ikifuatiwa na Tanzania iliyopo nafasi ya 117 Sudani Kusini iliyopo katika nafasi ya 118, Burundi nafasi ya 119, Somalia nafasi ya 126, D R Congo nafasi ya 130 Uganda nafasi ya 131, na Rwanda ikiwa ya mwisho kwa kanda hiyo katika nafasi ya 139 (39.58%).
RSF inabainisha kuwa kwa ujumla, nchi za EAC bado zinakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kulinda uhuru wa vyombo vya habari, ikiwemo shinikizo la kisiasa, mazingira magumu ya kazi kwa wanahabari, na vikwazo vya kisheria katika baadhi ya nchi.