Janeth Ritte
WAZIRI Kivuli wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wa ACT Wazalendo, Janeth Ritte, ameikosoa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile alichodai ni kutotoa kipaumbele cha kutosha kwa masuala ya watoto katika bajeti ya Serikali. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Akitoa maoni kuhusu bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 Janeth alisema kuwa licha ya Mwenyekiti wa CCM, Samia Suluhu Hassan, kueleza kuwa watoto watatengenezewa mazingira na huduma bora zaidi, bado bajeti iliyowasilishwa haijaonesha fungu maalumu kwa ajili ya watoto.
Aidha, alisema kuwa hata katika mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, hakuna mpango unaoonekana wazi unaolenga kuwahudumia watoto, jambo ambalo kwa mujibu wake linaonesha kuwa mahitaji ya kundi hilo hayajapewa uzito unaostahili.
Janeth ameitaka Serikali kuhakikisha masuala ya watoto yanapewa nafasi ya pekee katika mipango na bajeti za maendeleo ili kulinda na kuendeleza ustawi wao.