SERIKALI itarajia kuanza kutoza ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia 5 kwenye thamani ya dau la kamari inayochezwa kwa njia ya michezo ya kubashiri ya ardhini au mtandaoni, michezo ya kasino ya ardhini au mtandanoni, mashine za sloti arobaini pamoja na michezo ya vikaragosi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Pendekezo hilo limetolewa bungeni, leo tarehe 11 Juni 2026 na Waziri wa Fedha Balozi Khamis Mussa Omar, wakati akisoma Hotuba ya Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2026/2027 ambapo amesema asilimia 10 ya mapato yatakayokusanywa kutoka kwenye chanzo hiki (ushuru wa asilimia 5) yatawasilishwa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT) ili kuongeza ufanisi katika udhibiti wa michezo ya kubahatisha.
Kama pendekezo hilo la Serikali litapitishwa na wabunge wanaotarajia kuanza kujadili bajeti hiyo, tarehe Juni 14, 2026 litaanza kufanya kazi tarehe 1 Julai, 2026.