England na Costa Rica zinatarajiwa kukutana Juni 10, 2026 saa 23:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaochezwa kwenye Uwanja wa Inter&Co Stadium, Orlando, Marekani.
Mchezo huu ni sehemu ya maandalizi ya mwisho ya England kuelekea Kombe la Dunia 2026, huku Costa Rica ikitumia nafasi hiyo kujipima dhidi ya moja ya timu bora duniani. England inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na kikosi chenye mchanganyiko wa uzoefu na vijana chini ya kocha Thomas Tuchel.
Nahodha Harry Kane anatarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji akisaidiwa na nyota kama Jude Bellingham na Bukayo Saka. Tuchel anaamini kuwa kuwa mechi hizi za kirafiki ni muhimu kwa kuwajengea wachezaji utayari wa kukabiliana na mazingira ya joto yatakayokuwepo katika Kombe la Dunia la mwaka huu.
Kwa upande wa Costa Rica, timu hiyo imekuwa ikipitia kipindi cha mabadiliko huku ikiwapa nafasi wachezaji vijana kujiandaa kwa mashindano yajayo. Hata hivyo, maandalizi yao yameathiriwa na kuondolewa kwa baadhi ya wachezaji kutokana na masuala ya kinidhamu, jambo ambalo linaweza kuathiri uimara wa kikosi chao dhidi ya England.
Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Kihistoria, timu hizi zimekutana mara mbili pekee. Mwaka 2014 zilitoka sare tasa katika hatua ya makundi ya Kombe la Dunia nchini Brazil, kabla England haijashinda mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki wa mwaka 2018. Takwimu hizo zinaonyesha England haijawahi kufungwa na Costa Rica, jambo linalowapa ari ya kuendelea kutawala rekodi hiyo.
Kimbinu, England inatarajiwa kumiliki mpira kwa kiwango kikubwa na kushambulia kupitia pembeni kwa kutumia kasi ya mawinga wake. Costa Rica huenda ikacheza kwa kujilinda zaidi na kutegemea mashambulizi ya kushtukiza. Kwa kuzingatia ubora wa vikosi, uzoefu wa wachezaji na maandalizi ya sasa, England inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi.