MAHAKAMA ya Rufani imepanga kusikiliza maombi ya Mkurugenzi wa makosa ya jinai(DPP) dhidi ya Tundu Lissu tarehe 6 Julai 2026,Awali mahakama ilipanga kusikiliza kesi hiyo tarehe 11 Juni 2026.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Maombi hayo yanatokana na upande wa mashtaka kutoridhishwa na uamuzi wa mahakama kuu wa tarehe 24 Februari 2026 ambapo mahakama iliamua kukubali hoja za Lissu kwamba ushahidi wa nyongeza wa kamishna wa Polisi Amini Mahamba haukubaliki kisheria kuingizwa mahakamani hapo.
Lissu anakabiliwa na kesi ya msingi ya Uhanini ambapo tayari Jamhuri ishawasilisha mashahidi zaidi ya 14.