MAELFU ya familia za wakulima wadogo wa kahawa nchini zinatarajiwa kuendelea kunufaika na programu za maendeleo kufuatia mabadiliko ya uongozi katika Hanns R. Neumann Stiftung (HRNS), taasisi ya kimataifa inayosaidia kilimo endelevu cha kahawa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
HRNS, ambayo imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na wakulima wa Tanzania hususan katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Kaskazini, imetangaza uteuzi wa Dk. Karen Hadem kujiunga na Jens Sorgenfrei katika uongozi wa taasisi hiyo, wakiahidi kuendeleza mafanikio yaliyowekwa na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji, Michael Opitz.

Kwa mujibu wa Meneja wa HRNS Tanzania, Morgan Mkonyi, uongozi mpya utaendelea kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali nchini ili kuongeza uzalishaji wa kahawa, kuboresha kipato cha kaya za wakulima, kuhifadhi mazingira na kuwapatia vijana fursa zaidi za maendeleo.
Ikiungwa mkono na mtaji wa kudumu wa takribani Euro milioni 150, HRNS imeahidi kuendelea kufadhili programu za muda mrefu zinazoboresha maisha ya jamii zinazolima kahawa duniani, ikiwemo Tanzania.