Dimba la bet365 litatawakutanisha wababe wawili kwenye mchezo wa raundi ya nne ya Championship kati ya Stoke City na Norwich City, saa 22:00 usiku. Timu zote mbili zinaingia mechi hii zikiwa kwenye nafasi za chini kwenye msimamo.
Stoke City wanaingia kwenye mechi hii wakiwa katika hali ngumu sana, wakiwa wameshindwa kupata ushindi kwenye mechi zote tatu za kwanza za Championship. Chini ya kocha Mark Robins, Stoke walianza kwa kupoteza dhidi ya Swansea, kisha wakapoteza dhidi ya Southampton, na hatimaye wakafungwa mabao 4-1 dhidi ya Wolves wikiendi iliyopita, licha ya Sam Gallagher kuwapa uongozi wa mapema katika dakika ya pili.
Kocha Robins amekuwa akitaja makosa ya kujitakia kama tatizo kuu la timu yake, na hadi sasa Stoke wameshapokea mabao nane katika mechi tatu tu za ligi na kushikilia nafasi ya mwisho ya msimamo.
Kwa upande wa Norwich City, hali ni tofauti kidogo. Ingawa walianza msimu kwa kufungwa 1-2 nyumbani dhidi ya West Bromwich Albion na kisha wakapigwa vibaya na Millwall, timu ya kocha Philippe Clement imeonyesha mwamko mkubwa hivi karibuni kwa kuipiga Burnley mabao 4-1.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Katika ushindi huo, Mohamed Toure alifunga mabao mawili, huku Andre Brooks akiongeza bao lingine, na mabao matatu yakiwa yamefungwa ndani ya dakika 21 za kwanza. Norwich pia walifanikiwa kuipiga Cardiff City 2-1 ugenini katika raundi ya pili ya Kombe la EFL wiki iliyopita.
Historia ya michezo ya hivi karibuni imeegemea zaidi upande wa Norwich, ambao wamekuwa wakitawala matokeo dhidi ya Stoke city licha ya kupoteza katika mchezo wao wa mwisho.
Kwa kuzingatia fomu tofauti kabisa ya timu hizi mbili Stoke wamekuwa na matatizo makubwa ya ulinzi na kupoteza mfululizo, huku Norwich wakiwa na kasi na kujiamini kutokana na ushindi wao wa hivi karibuni, Stoke pia wanakabiliwa na changamoto za majeraha akiwemo za Lamine Cissé, Junior Tchamadeu, Ato Ampah, na Aaron Cresswell, jambo linaloweza kuathiri zaidi muundo wao wa ulinzi.